Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - Mufti wa Tanzania Shekh Abubakar bin Zuber ametangaza kuwepo kwa dua kubwa ya kuiombea nchi, Rais pamoja na wazee wetu waliotangulia mbele ya haki.
Dua hiyo inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu mfululizo Kwa maana tarehe 8/9/10 mwezi wa tano 2025, katika Msikiti Mkuu wa Bakwata Kinondoni kwa siku mbili na kilele itakuwa tarehe kumi Jijini Dar.
Akitoa taarifa Kwa wanahabari Leo april 16 mchana huu alisema.... Nichukue nafasi hii kutoa taarifa ya kwamba tutakuwa na duwa kubwa ya kuiombea nchi Aman utulivu na kufungamana na tukio la kuwaombea wazee wetu waliotangulia mbele ya haki. Pamoja na Mamuft wetu Shekh Hemedi bin Jumaa na Mufti Simba.
Mbali na hao pia wazee waliopigania Dini kwa hali na mali. Jambo hili ambalo lilianza rasmi Mwaka Jana ni muendelezo wa kila Mwaka chini ya Usimamizi wa Bi Mwantumu Mahiza na Alhaji Sued Twaibu ambao ndio waanzilishi wa jambo hili
Katika mkutano huo wa Leo Mufti alikuwapo na Viongozi wakuu wa Bakwata pamoja na Viongozi wa Serikali kwa maana Wakuu wa Wilaya ya Ilala Kigamboni Temeke.
Your Comment